Hosea 2:5-10


5 aMama yao amekosa uaminifu
na amewachukua mimba katika aibu.
Gomeri alisema, ‘Nitawaendea wapenzi wangu,
ambao hunipa chakula changu
na maji yangu,
sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu
na kinywaji changu.’

6 bKwa hiyo mimi Mungu nitaizuia njia yake
kwa vichaka vya miiba,
nitamjengea ukuta ili kwamba
asiweze kutoka.

7 cGomeri atawafuatia wapenzi wake lakini hatawapata;
atawatafuta lakini hatawapata.
Kisha atasema,
‘Nitarudi kwa mume wangu kama kwanza,
kwa maana nilikuwa na hali njema zaidi
kuliko sasa.’

8 dGomeri hajakubali kuwa mimi ndiye
niliyempa nafaka, divai mpya na mafuta,
niliyemwongezea fedha na dhahabu waliyoitumia
kwa kumtumikia Baali.


9 e“Kwa hiyo nitachukua nafaka yangu wakati itakapokomaa
na divai yangu mpya wakati itakapokuwa tayari.
Nitamnyang’anya sufu yangu na kitani yangu
iliyokusudiwa kufunika uchi wake.

10 fBasi sasa nitaufunua ufisadi wake
mbele ya wapenzi wake;
hakuna yeyote atakayemtoa
mikononi mwangu.
Copyright information for SwhKC